NEWS

Wednesday 22 March 2023

Mwenyekiti wa Wazazi CCM Taifa akagua miradi ya maendeleo Tarime



Na Mara Online News
-----------------------------------

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya (pichani juu kushoto), leo ameendelea na ziara ya kikazi mkoani Mara, ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika majimbo ya Tarime Vijijini na Tarime Mjini.

Baadhi ya miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nyasaricho uliogharimu shilingi bilioni moja zilizotoletwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Maganya pia amekagua ujenzi wa soko la kisasa katika mji wa Tarime na kueleza kuridhishwa na ubora wa mradi huo na mingine inayotekelezwa na Serikali katika halmashauri zote mbili za Tarime Vijijini na Tarime Mji.

Katika ziara hiyo Maganya ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho tawala, amefuatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi.


Viongozi walioshiriki ziara hiyo ni Wabunge Mwita Waitara wa Tarime Vijjini na Michael Kembaki wa Tarime Mjini, Wenyeviti wa Halmashauri, Simion Kiles wa Tarime Vijijini) na Daniel Komote wa Tarime Mji, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chonchorio, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Marwa Daudi Ngicho na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele, miongoni mwa wengine.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages