NEWS

Tuesday 18 July 2023

Benki ya Azania Serengeti yawapa vijana mkopo wa bodaboda kwa riba nafuu


Sehemu ya vijana wakiwa na bodaboda walizopewa mkopo kutoka Benki ya Azania Tawi la Serengeti kwa riba nafuu ya asilimia 2.

---------------------------------------------------
Na Mwandishi wa

Mara Online News
-------------------------

BENKI ya Azania Tawi la Serengeti imewapa vijana mkopo wa pikipiki za abiria (bodaboda) 13 kwa riba nafuu ya asilimia mbili ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi. 

 
Vijana waliopata mkopo huo ni wanachama wa vikundi vya MCU na Serengeti Home Centre.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi bodaboda hizo kwa vijana hao mjini Mugumu leo, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Serengeti, Dkt Vincent Mashinji ameishukuru benki hiyo kwa kuonesha mfano mzuri unaostahili kuigwa na wadau wengine wa maendeleo.

Aidha, DC Mashinji ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, ametumia nafasi hiyo pia kutoa wito wa kuhamasisha watu wa rika mbalimbali kuchangamkia fursa zinazopatikana katika Benki ya Azania kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.


DC Mashinji akikagua mojawapo ya bodaboda zilizotolewa na Benki ya Azania Tawi la Serengeti mkopo wenye riba nafuu.

Naye Meneja wa Benki ya Azania Tawi la Serengeti, Elizabeth Koboko ametoa wito wa kuwakaribisha wananchi katika benki hiyo ili kupata huduma bora za kifedha na mikopo ya kujikwamua kimaisha.

Kwa upande wao, vijana waliopata mkopo huo wa bodaboda wameishukuru Benki ya Azania Tawi la Serengeti, huku wakiahidi kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa kupitia shughuli za usafirishaji abiria.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages