NEWS

Monday 3 July 2023

Serikali, Barrick wawatangazia wananchi Nyamichele, Murwambe malipo ya kifuta jashoMakamu Meneja wa Idara ya Mahusiano katika Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara, Hermence Christopher Lulah (aliyesisimama) akizungumza katika mkutano wa kijijini Nyakunguru (Nyamichele). Waliokaa mbele kutoka kuchoto ni Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya, James Yunge.

Na Mwandishi wa

Mara Online News
--------------------------

SERIKALI imewatangazia wananchi wa maeneo ya Nyamichele na Murwambe wilayani Tarime utaratibu wa kuanza kuwalipa kifuta jasho baada ya Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara kusitisha mpango wa kuyachukua.

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, James Yunge ametangaza katika mikutano ya hadhara iliyofanyika vijiji vya Kewanja (Murwambe) na Nyakunguru (Nyamichele) kwa nyakati tofauti leo Julai 3, 2023 kwamba Serikali imeidhinisha Kampuni ya Barrick kuwalipa wananchi hao kifuta jasho haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo Yunge ambaye ni Afisa Tarafa ya Ingwe ulipo mgodi wa Barrick North Mara, amesema malipo hayo yataanza kutolewa wakati wowote wiki hii baada ya Mkuu wa Wilaya kuunda timu maalum ya kusimamia shughuli hiyo.Mikutano hiyo imehudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara ambaye amewahimiza wananchi hao kujitokeza kuchukua malipo yao kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.

Makamu Meneja wa Idara ya Mahusiano katika Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara, Hermence Christopher Lulah amesema wananchi takriban 3,000 kutoka maeneo ya Murwambe na Nyamichele wameorodheshwa kwa ajili ya kulipwa kifuta jasho.

“Malipo yataanza kulipwa haraka iwezekanavyo, na tunafikiria kutumia utaratibu wa kuweka fedha moja kwa moja kwenye akaunti za wahusika badala ya kuwaandikia hundi ili kuepusha ucheleweshaji,” amesema Hermence.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages