NEWS

Wednesday 10 April 2024

Serikali ya Tanzania yatangaza mabadiliko ya jina la Tume ya UchaguziNa Mwandishi wa
Mara Online News
-----------------------------


SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza mabadiliko ya jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambapo sasa itajulikana kwa jina la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali imesema jina la INEC litaanza kutumika rasmi kuanzia Aprili 12, 2024.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mabadiliko hayo yamefanyika kufuatia Tangazo la Serikali Na. 225 la tarehe 29 Machi, 2024, Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages