NEWS

Friday 12 April 2024

Gari la Shule ya Ghati Memorial ladumbukia korongoni, wanafunzi 7 wahofiwa kufa




Na Mwandishi Wetu, Arusha
---------------------------------------


WANAFUNZI saba wa Shule ya Msingi Ghati Memorial wanahofiwa kufa baada ya gari lao (pichani juu) kudumbukia kwenye korongo lililojaa maji eneo la Dampo mkoani Arusha.

Ajali hiyo imetokea saa 12 asubuhi leo Aprili 12, 2024, ikidaiwa kuwa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili T 496 EFK alipoona ameshindwa kulidhibiti aliruka na kuliacha likidumbukia korongoni.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, wanafunzi wanne na walimu wawili wameokolewa na kwamba juhudi za kuwatafuta wanafunzi saba zinaendelea.

Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Arusha, Osward Mawanjejele amethitibisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba taarifa za awali alizopata zinaeleza kuwa gari hilo lilikuwa limebeba wanafunzi 11 na walimu wawili.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa dereva wa gari hilo alionywa na waendesha bodaboda waliokuwa eneo hilo wakimsisitiza asivuke kwani kasi ya maji ilikuwa kubwa, lakini akalazimisha kupita.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages