
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Mugini Jacob (wa nne kutoka kushoto) ameongoza kikao cha Kamati Tendaji ya klabu hiyo jijini Mwanza leo Agosti 6, 2024.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho ambacho kimefanyika kwenye Hoteli ya Aden Palace, kimeazimia yafanyike maboresho ya mifumo ya matumizi ya fedha na kuongeza vyanzo vya mapato ya MRPC.
Aidha, kikao hicho kimeongeza muda wa siku 30 kwa ajili ya wanachama wa klabu hiyo ambao hawajalipa ada ya mwaka huu kuhakikisha wanalipa.
“Tumezungumzia masuala muhimu ya kuendeleza MRPC, na kuhusu suala la wanachama ambao hawajalipa ada tumewaongezea mwezi mmoja ili waweze kulipa,” amesema Jacob.

Mwenyekiti wa MRPC, Mugini Jacob akiwasili Aden Palace Hotel kwa ajili ya kushiriki kikao hicho cha Kamati Tendaji ya klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment