NEWS

Tuesday, 6 August 2024

Kamala Harris amtangaza Tim Walz Kuwa mgombea mwenza Wake Katika Kinyang'anyiro cha Urais

Bi Harris kamala pamoja na mgombea mwenza Bw.Tim Walz
                                                                 
Kamala Harris amemchagua gavana wa Minnesota Tim Walz, kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa rais wa Marekani, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.

Bi Harris na mgombea mwenza wake wanatarajiwa kuanza ziara ya kampeni katika majimbo yanayosadikiwa kuwa na ushindani mkali, mkutano wa kwanza ukipangiwa kufanyika huko Philadelphia baadaye leo.

Kura ya maoni ya hivi punde ya kituo cha CBS, mshirika wa BBC wa Marekani, inawaonyesha Bi Harris na Trump wakiwa katika kinyang'anyiro kikali kitaifa, huku Mgombea huyo wa chama cha Democratic akiongoza kwa pointi moja dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump.
                                                      CHANZO:BBC
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages