
Mbunge Mwita Waitara
NA MWANDISHI WETU, Musoma
MBUNGE wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, ametoa kauli kali dhidi ya kamati za siasa za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Mjini na Tarime mkoani Mara, akisema kuwa angekuwa na mamlaka, angezivunja mara moja.
“Ningekuwa na uwezo, ningefuta Kamati ya Siasa ya Musoma Mjini, ningefuta Kamati ya Siasa ya Tarime… it is very unfair,” Waitara alisema kwa hisia kali.
Waitara alitoa kauli hiyo wakati akizungumza mjini Musoma jana katika mkutano wa hadhara wa wananchi ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vedastus Mathayo (CCM).
Aliendelea: “Ukitaka kufanya siasa safi hapa mkoa wa Mara ni lazima tuambiane ukweli – kama ni jipu tulitoboe – tulikamue tutoe kiini.”
Kauli hiyo ya Waitara imeibua maswali mengi miongoni mwa wachambuzi wa siasa na wanachama wa CCM, ikitafsiriwa na baadhi kuwa ni dalili za mvutano wa ndani kwa ndani kuhusu namna siasa inavyoendeshwa katika majimbo ya Musoma Mjini na Tarime.
No comments:
Post a Comment