NEWS

Wednesday 15 April 2020

Mahabusu, mfungwa Butimba wauawa wakijaribu kutoroka


Mahabusu wawili na mfungwa kutoka Gereza Kuu Butimba mkoani Mwanza wameuawa kwa kipigo na risasi walipojaribu kutoroka chini ya ulinzi.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Muliro Muliro leo Jumatano Aprili 15, 2020 amewataja mahabusu waliouawa kuwa ni Yusuph Benard (34) na Seleman Seif (28) waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji.

 Kamanda Muliro amemtaja mfungwa aliyeuawa kuwa ni George Aloyce (34) aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 15 kwa kosa la uhujumu uchumi, lakini pia cha miezi sita kwa kujaribu kutoroka chini ya ulinzi.

 Amefafanua kuwa mahabusu hao walifariki dunia jana Jumanne saa 12:30 jioni katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza – Sekou Toure walikopelekwa kutibiwa mara baada ya kushambuliwa na raia walioshirikiana na askari magereza kuwadhibiti walipojaribu kutoroka gerezani.

 Kwa mujibu wa Kamanda Muliro, mfungwa huyo naye alifariki dunia siku hiyo katika hospitali hiyo kutokana na majeraha ya risasi aliyopata miguuni, zilizofyatuliwa na askari alipojaribu kuwatoroka eneo la Mabatini jijini hapa.

(Habari na Christopher Gamaina, Mwanza)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages