
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho (wa tano kutoka kushoto mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Bunge na Menejimeti ya Shirika la Mzinga, Morogoro juzi.
Morogoro
-------------------
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), juzi ilifanya ziara ya siku moja ya kutembelea Shirika la Mzinga lililopo mkoani Morogoro, kwa lengo la kujionea jinsi linavyotekeleza majukumu yake ya msingi.
Shirika la Mzinga ni moja ya mashirika makubwa ya kimkakati yaliyo chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Mashirika mengine ni NYUMBU na SUMAJKT.
Ujumbe wa Kamati hiyo ya NUU iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Najma Giga, ulipokewa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji Mnyepe.
Menejimenti ya Shirika la Mzinga iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Luteni Jenerali mstaafu Balozi Charles Makakala pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Brigedia Jenerali Seif Hamis.

Waziri Nyansaho akizungumza katika kikao cha majumuisho
Kamati hiyo ya Bunge ilipata wasaa wa kutembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda, likiwemo la mkondo wa uzalishaji mazao ya msingi.
Akizungumza na uongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa majumuisho mara baada ya kutembelea maeneo ya uzalishaji wa mazao ya msingi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Giga, alilipongeza shirika hilo kwa namna linavyotekeleza majukumu yake kwa weledi katika uzalishaji mali na kuendelea kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake mwaka 1971.
Giga aliongeza kuwa lengo la ziara hiyo ya kamati yake ni kuona jinsi Shirika la Mzinga linavyotekeleza majukumu yake na kama linakabiliwa changamoto katika utekelezaji wa majukumu hayo na kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment