
Wafanyakazi wanawake wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara wakifurahia jambo katika hafla ya Siku ya Wanawake Duniani 2026.
Wafanyakazi wanawake wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara wamesema wanajivunia juhudi zinazofanywa na mgodi huo katika kuboresha afya, usalama na uwezeshaji wanawake kazini.
Wamesema kupitia mipango na fursa mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya Barrick wameweza kuimarishiwa mazingira ya kazi yenye ushirikishwaji.

Wafanyakazi wanawake hao wa Barrick North Mara waliyasema hayo hivi karibuni katika taarifa yao ya mafanikio kazini kwa mwaka 2025, wakati wa hafla iliyofanyika mgodini hapo kusheherekea Siku ya Wanawake Duniani, mwaka huu.

Wafanyakazi wa Barrick North Mara wakipiga makofi katika hafla hiyo
Taarifa ilisema wafanyakazi wanawake wa mgodi huo walipata mafanikio makubwa katika kipindi cha mwaka 2025.
“Tunathamini mchango endelevu wa uongozi katika kuboresha ustawi wa wafanyakazi na kuongeza fursa kwa wanawake ndani ya kampuni,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
GM Lyambiko akikabidhi cheti kwa mmoja wa wanawake hao wakati wa hafla hiyo
Wanawake hao walisema pia wamepata mafunzo ya afya ya uzazi ambayo yalijumuisha wafanyakazi wanawake na wakandarasi wa Barrick North Mara.
Kwenye medani ya kimataifa, taarifa hiyo iligusia ushiriki wa wafanyakazi wanawake wa Barrick North Mara katika Mkutano wa Wanawake wa Afrika katika masuala ya Mazingira, Afya na Usalama (African Women in EHS Conference).
Mkutano huo uliwawezesha kupata uzoefu, maendeleo ya kitaaluma, kujenga uwezo wa uongozi na mahusiano mapya.

Meneja Msaidizi wa Idara ya Mahusiano wa Barrick North Mara, Nasieku Kisambu, akisisitiza jambo katika hafla hiyo.
Kwa upande mwingine, taarifa hiyo ilisema wafanyakazi wanawake na wakandarasi 48 kutoka Barrick North Mara walishiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2026 yaliyofanyika kimkoa katika mji wa Mugumu, wilayani Serengeti, ikiwa ni sehemu ya msisitizo wa kampuni wa kuendeleza usawa wa kijinsia wa kutaka wanawake kujuimuika na jamii.
Wafanyakazi wanawake wa Barrick North Mara wakicheza katika hafla hiyo

Sehemu ya wanafanyakazi wa Barrick North Mara kwenye hafla hiyo
Taarifa hiyo iliongeza kuwa mgodi huo pia umeendelea kufanya kazi nzuri kuboresha vyumba vya makazi ya wafanyakazi wanawake.
Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaendeshwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals.

Wafanyakazi wa Barrick North Mara wakifurahia jambo katika hafla hiyo


No comments:
Post a Comment