Kutoka kulia : Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime Mkaruka Kura, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime Marwa Daudi Ngicho, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Tarime Godfrey Francis na Katibu hamasa chipukizi Mkoa wa Mara Mossy Magele.
Na Clonel Mwegendao, Tarime
Uongozi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Tarime umeapa
kutofumbia macho viongozi wa upinzani wanaotukana viongozi wa serikali ya chama
hicho na kupotosha wananchi kwa maneno ya uongo
Akizungumza katika kikao cha baraza la kawaida la UVCCM uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za chama hicho wilaya Mwenyekiti a CCM Wilaya ya Tarime Marwa Daudi Ngicho amekemea vikali tabia ya baadhi
ya viongozi wa upinzani kutoa maneno makali na yasiyokuwa ya kweli dhidi ya
viongozi CCM nakuhaidi kuchukua hatua kali dhidi kiongozi yoyote atakayemchafua Rais Magufuli kwani kiongozi huyo ameweza kufanya maendeleo makubwa na yanaonekana.
Aidha amewataka vijana wote kufanya kazi kwa bidii katika
kulinda na kutunza heshima ya CCM ikiwa ni pamoja na kumuenzi
rais wa kwanza wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati mwalimu Julius
Kambarage Nyerere
“Fanya kazi kama mtumwa ili badae uishi kama mfalme hivyo tufanye
kazi kwa bidii ili tuondoe upinzani Tarime ili tuishi kwa amani na kuharakisha maendeleo yetu”alisema
Ngicho.
No comments:
Post a Comment