NEWS

Friday 19 July 2019

DC KABEHO ATAKA TARIME MPYA ISIYO KUWA NA UKATILI


Mkuu Wa Wilaya ya Tarime Charles Kabeho akisisitza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza  vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake  uliofanywa na shirika la Kivulini katika kijiji cha Magoma leo.  Wkwanza  kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime (DAS) John Marwa .( Picha na Mara Online)




















Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime(DC) Charles Francis Kabeho amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuachana na mila kandamizi ikiwemo ukeketaji  na ndoa za utotoni.

DC Kabeho ametoa agizo hilo leo wakati  akizindua  ya kampeni ya kupinga ukatili kwa akina mama na watoto  katika kijiji cha Magoma nje kidogo ya mji wa Tarime.

“Tunataka tuwe na Tarime mpya isiyokuwa na ukatili wa aina yoyote na kuanzia leo kauli mbiu ya kupinga ukatili  wa akina mama na watoto ningependa  iwe ,Tarime mpya ukatili wa akina mama na watoto haiwezekani” alisema Kabeho.
Uzinduzi huo wa kupinga ukatili kwa mwaka 2019/2019 uliandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Kivulini.
Kabeho aliahidi pia kufuatilia ucheleweshaji wa kesi zinazohusu ukatilii.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa  Kivulini Yassin Ally alitumia fursa hiyo pia kuwaomba wananchi wa Tarime kuwekeza katika elimu ya watoto wao bila kujali jinsia kwa faida yao na taifa kwa ujumla. 
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wazee wa mila, wanafunzi, mashirika yanayotetea haki za watoto na wanawake na maofisa wa serikali kutoka idara zinashughulikia masuala ya ukatili.





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages