Na Clonel Mwegendao
Wanafunzi wa shule ya sekondari Ngoreme iliyopo katika kata
ya Kenyamonta wilayani Serengeti mkoani Mara wamekuwa wakitembea umbali wa
takribani kilomita 12 kufika katika
shule hiyo jambo ambalo limekuwa likipelekea baadhi ya wanafunzi kukosa masomo na kutopenda shule.
Akizungumza na Mara Online News leo kwa njia ya simu diwani
wa kata ya Kenyamonta Sosteness Mwigicho Samwel amesema kuwa mpaka sasa kwa
kushirikiana na wananchi pamoja na serikali wamefanikiwa kujenga hosteli ya
kisasa kwa ajili ya wavulana na wasichana yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 120
wakiwemo wavulana 80 na wasichana 40.
Hata
hivyo ameweza kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha katika
kufanikisha ujenzi wa hosteli hiyo na kutoa wito kwa
jamii kuweka kipaumbele katika elimu ili kupata vijana wenye weledi jambo
ambalo litasaidia kuwa na vijana wenye uwezo wa kuleta maendeleo katika jamii
na taifa
No comments:
Post a Comment