Wananchi wa kata ya Kenyamonta Wilayani Serengeti wanakabiliwa na uhapa wa maji safi na salama baada ya mashine iliyokuwa inatumika kusukuma maji kuharibika.
Diwani wa kata hiyo Sostenes Samwel amesema wananchi wa kata yake sasa wanatumiwa maji maji ya bwawa ambayo sio safi na salama.
‘’Kwakweli tatizo la maji sasa limegeuka kuwa
ker okubwa kwa wananchi wa kata ya Kenyamonta. Naiomba serikali na wadau
wengine wa maendeleo watusadie ili wananchi wapate maji safi na salama”, Samwel
ameambia Mara Online News leo .
Amesema maeneo mengi ya kata hiyo hayana
miundombinu ya maji .
Hata hivyo diwani huyo ametoa wito kwa wananchi
wa kata hiyo kuendelea kuchemsha maji ya kunywa wakati juhudi zikutatua tatizo
la maji zinaendelea katika kata hiyo.
.(Na Clonel Mwegendao, Serengeti)
No comments:
Post a Comment