NEWS

Tuesday 10 September 2019

FARU TISA WATUA SERENGETI KUTOKA AFRIKA KUSINI


Ushirikiano mzuri kati ya Serikali ya Tanzania na Taasisi ya Grumeti Fund umefanikisha kuhamisha faru weusi tisa kutoka Afrika Kusini kuja Serengeti.
Faru hao wamewasili salama leo(Jumanne) asubuhi kwa  ndege kubwa ya mizigo katika maeneo ya  hifadhi ya Grumeti .
Mkuu wa Mkoa wa Mara(RC) Adam Malima ameongoza hafla ya mapokezi ya faru hao.


 “ Tunataka afaru waongezeke Serengeti na tusijekujaribishana kwa hili”, Mkuu wa Mkoa alionya mara baada ya kupokea faru hao.
 Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Mara na Wilaya ya Serengeti walihudhuria mapokezi ya faru  hao.
Hafla hiyo pia ilihudhuhuriwa  na wahifadhi  wa wanyamapori kutoka taasisi mbalimbali za serikali na Grumeti Fund.
 Tumepokea faru hawa na tunawapeleka mbugani hili ni jukumu kubwa  na ndio maana hata mapokezi yake sio kitu kidogo”, alisema RC Malima.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alishukuru serikali ya Tanzania na taaisi ya Grumeti Fund kwa kufanikisha kuwaleta faru hao Serengeti.
Grumeti Fund ni taasisi inayojihusisha na uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya jamii katika mapori tengefu ya Ikorongo- Grumeti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Grumeti Fund Stephen Cunliffe alisema ushirikiano mzuri kati ya Serikali ya Tanzania na taasisi ya Grumeti Fund  umefanikisha kuhamisha faru hao weusi  kutoka Afrika Kusini kuja Serengeti.
Cunliffe alisema taasisi hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kuongeza  faru weusi  katika ikolojia ya Serengeti.

1 comment:

  1. Safi saana siku moja Serengeti itakuwa kivutio bora dunian zaid ya sasa

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages