Mkoa wa Mara umepanga kupanda miti 100,000 katika Maadhimisho ya nane ya siku ya Mara ambayo mwaka huu(2019) yatafanyika nchini Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Mara(RC) Adam Malima amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake leo Septemba 03 kuwa maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia Septemba 12-15 katika viwanja vya Sokoine mjini Mugumu, Wilayani Serengeti.
Mbali na shughuli za upandaji miti, RC Malima amesema kutakuwepo na maonesho ya bidhaa mbalimbali yatakayohusisha wananchi na wadau wengine wa maendeleo .
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kauli mbiu ya Siku ya Mara Mwaka huu ni “ Mimi Mto Mara Nitunze Nikutunze”,
Aidha RC Malima amesema Septemba 14 kutakuwepo na kongamano muhimu ambalo litahusisha wadau wakubwa wa bonde la mto Mara kutoka Tanzania na Kenya.
Shughuli nyingine ambayo itakayofanyika katika maadhimisho hayo ni uwekaji wa lama za mipaka(beacons) katika mipaka ya bonde la mto Mara na vijiji jirani.
RC Malima amesema pia kutakuwepo na mashindano ya michezo mbalimbali katika maadhimisho
hayo.
RC Malima amesema pia kutakuwepo na mashindano ya michezo mbalimbali katika maadhimisho
hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara akisisitiza umuhimu wa Maadhimisho ya siku ya Mara katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake |
Viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka mataifa hayo mawili wanatajaria kuhudhuria katika maadhimisho hayo ambayo kilele chake itakuwa ni Septemba 15 , amesema Mkuu wa Mkoa .
Tanzania na Kenya huadhimisha siku ya Mara Septemba 15 kila mwaka kwa kupokezana ikiwa ni sehemu ya kuendeleza juhudi za uhifadhi endelevu katika bonde la Mto Mara.
Kwa kutambua umuhimu wa ikolojia ya Mara , kikao cha 10 cha Sekretarieti ya Mawaziri wa Bonde la Ziwa Victoria kilichofanyika Kigali nchini Rwanda Mei 4,2012 kiliazimia Septemba 15 kila mwaka kuwa siku ya Mara .
Maadhimisho ya kwanza ya siku ya Mara yalifanyika 2012 nchini Kenya na kwa upande wa Tanzania maadhimisho ya kwanza ya siku ya Mara yalifanyika 2013 .
TAZAMA VIDEO
No comments:
Post a Comment