NEWS

Monday, 23 September 2019

WALIOFARIKI AJALI YA NDEGE SERENGETI


  
Na Mwandishi Wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti  Nurdin  Babu ametaja mahemu waliofariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea  leo asubuhi(Septemba 23,2019)  katika uwanja mdogo wa  ndege wa Seronera   kuwa ni Nelson  Mabeyo(24) na Nelson Ulotu ambaye pia  ana umri unaokaribiana na mwenzake . 

“Nelson Mabeyo alikuwa ni rubani  na Nelson Ulotu alikuwa ni msaidizi wake(co-pilot)”, DC Babu ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio leo mchana.

“ Tumefika eneo la ajali na daktari ameifanyia mili "treament" na sasa tunasuburi helikopita inakuja kchukua mwili wa Nelson Mabeyo  na mwili mwingine  unafuatwa na ndege ya kampuni ya Auric Air”, amesema Mkuu huyo wa Wilaya ambaye alizuru katika eneo la ajali akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya  ya Serengeti.

Ndege  hiyo ilipata ajali  saa moja asubuhi wakati ikiwa katika harakati za kuruka  kutoka Seronera kuelekea kirawila kuchukua watalii .

Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) limethibithisha kutokea kwa ajali hiyo kupitia akaunti yake ya twetter muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea.
Mwisho ,.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages