Na mwandishi wetu, Nairobi
Watanzania wanaoishi nchini Kenya , mabalozi wa kutoka mataifa mbalimbali na wananchi wa Kenya jana Jumamosi Septemba 12, 2019 waliungana
na watanzania kuadhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere .
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dr Pindi Chana aliongoza maadhimisho hayo ambayo pia yalihudhuriwa na mwanasheria maarufu wa Kenya Profesa Patrice Lumumba.
Profesa Lumumba alisema Mwalimu Nyerere alikuwa nia
mwaharakati na mkombozi wa kweli kwa baara la Afrika.
Aidha Profesa Lumumba alisema Mwalimu Nyerere alikuwa ni moja ya viongozi
waliaonzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt
Chana aliwashukuru wote walioungana na watanzania kuadhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya Mwalimu Nyerere.
Dr Chana alisema Mwalimu Nyerere ameendelea kubaki kuwa ishara ya upendo sio tu kwa Tanzania bali kwa bara zima la Afrika.
“ Mwalimu alitufundisha, umoja, upendo, mshikamano
na alitufundisha kuwa rushwa ni adui ya haki. Leo hii ni miaka 20 bila Mwalimu
lakini kutokana na mawaidha na maneno yake
ni kama tupo naye hadi leo”, alisema Dr Chana.
No comments:
Post a Comment