Na Raphael Okello, Bunda
VIJANA nchini wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na serikali
ya awamu ya tano katika kubuni nafasi za ajira kwa kutumia vipaji
vyao badala ya kuendelea kulalamikia nafasi za ajira.
Rai hiyo imetolewa jana na Mwanaharakati Huru nchini, Cyprian
Musiba, alipokuwa akikabidhi zawadi mbalimbali kwa vijana baada ya
mashindano ya Kombe la Magufuli(Magufuli Cup) yaliyofanyika katika
viwanja vya Kibara jimbo la Mwibara wilayani Bunda mkoani Mara.
Musiba alisema kuwa Rais Magufuli katika awamu ya uongozi
anatekeleza miradi mikubwa na midogo kwa lengo la kutoa fursa kwa
vijana na kwamba ni juhudi za vijana kutumia fursa hizo kujikomboa
kiuchumi na kuwataka vijana kuchapakazi na kuacha kujiingiza
katika matumizi ya madawa ya kulevya.
.
“Lengo la mashindano haya ya ‘Magufuli Cup’ ni kupongeza na kuunga
mkono juhudi hizi zote za Rais Magufuli katika kuifikisha Tanzania
katika uchumi wa kati.
Akizungumzia siku ya ukumbusho ya kifo cha Baba wa Taifa hayati
Mwalimu Julius Nyerere, Musiba alisema , Rais Dkt. Magufuli
anamuenzi Baba wa taifa kwa kufanya yote aliyoanzisha katika taifa
hili kipindi cha uhai wake jambo ambalo hakuna Mtanzania mwenye nia
njema na nchi yake anayeweza kupinga.
No comments:
Post a Comment