NEWS

Tuesday 15 October 2019

SERENGETI YATOA SHULE MBILI ZA KWANZA KITAIFA

 Na Mwandishi Wetu,Serengeti.

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imefanikiwa kutoa  shule mbili  za kwanza bora kitaifa  katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2019 ambapo nafasi ya kwanza  imeshikwa na shule ya msingi  Graiyaki ikifuatiwa na shule ya msingi Twibhoki zote za Mjini Mugumu, Serengeti Mkoani Mara . Grace Imori Kutoka shule ya msingi Graiyaki  ametangazwa kuwa mwanafunzi wa kwanza kitaifa katika matokeo hayo ambayo yametangazwa leo na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages