Na Amina Kakiva,
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samwel Kiboye Namba
Tatu jana ametunukiwa cheti na taasisi
ya Professor Mwera Education Foundation kwa kutambua mchango wake anaoutoa katika
maendeleo ya jamii .
Mwenyekiti huyo alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya kidato cha nne katika
shule ya sekondari ya wasichana ya Tarime.
Katika hotuba yake
Namba tatu aliwaonya vikali vijana wanaoendesha bodada kuacha kuwarubuni
wanafunzi wa kike jambo ambalo linakatisha ndoto zao kielimu.
Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mara
kuwapatia fursa watoto wa kike kusoma baadala ya kuwaozesha mapema kwa lengo la
kupata mahari .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Professor Mwera
Education Foundation Peter Mwera alisema uwekezaji katika elimu ya vijana ni
jambo linalopaswa kupewa umuhimu mkubwa.
Jumla ya wanafunzi wa kike 44 walitunukiwa vyeti vya kihitimu elimu katika mahafali hayo.
No comments:
Post a Comment