NEWS

Wednesday 16 October 2019

REAL MADRID YA ZINEDINE SASA YAAMUA KUFANYA KUFURU YA USAJILI



 

Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86, kwa Mcolombia James Rodriguez mwenye umri wa miaka 28, anayecheza safu ya kati ili kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Chelsea Mfaransa N'Golo Kante. (El Desmarque, via Sport Witness.

Mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 33, anasakwa na Manchester United lakini ameonywa kuwa atahitaji kushusha kiwango cha madai yake ya mshahara. (ESPN)

Hata hivyo Manchester United, wanahofu kuhusu ugumu wa kusaini mkataba mpya wowote na wachezaji wapya katika kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi Januari . (Metro)

Kocha wa Arsenal Unai Emery, hatazamii kupanua kikosi chake mwezi Januari wakati wa kipindi cha uhamisho wa wachezaji. (The Athletic, via Mirror)

Tottenham Hottspurs, wameimarisha haja yao ya kumtaka Jose Mourinho huku kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu msimamo wa Manchester United wa kumtaka Mauricio Pochettino. (Daily Express)

Mshambuliaji wa Chelsea Mfaransa Olivier Giroud,mwenye umri wa miaka 33, anajiandaa kuondoka katika klabu hiyo mwezi  Januari ikiwa hatacheza tena. Inter Milan na timu ya Ligi kuu ya Canada Vancouver Whitecaps ni miongoni mwa timu zinazomtaka. (Sun)

Manchester United wanamtaka Mario Mandzukic ashushe viwango vya mshahara ili wamuajiri Mchezaji wa safu ya kati wa Croatia Luka Modric amemuomba mchezaji mwenzake katika kikosi cha Real Madrid Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 30, akimtaka abakie katika klabu baada ya mshambuliaji huyo wa kati wa Wales kukaribia kabisa kuhamia Bernabeu msimu uliopita. (Independent)

Kiungo wa kati Mbrazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 27, bado anaweza kurudi Liverpool  ikiwa Bayern Munich wataaamua kutosaini mkataba wa kudumu na yeye msimu ujao, Kwa sasa anacheza kwa mkopo katika timu hiyo ya Ujerumani kutoka Barcelona. (AS, via TeamTalk)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages