Akiongea katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo, Ntiruhungwa amesema wanafunzi 2,000 wanatarajia kijiunga kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za serikali zilizopo katika mji huo wa Tarime.
Amesema upungufu uliopo ni vyumba takribani 15 vya madarasa na kusisitiza kuwa lazima watoto wote waliofaulu wajiunge na elimu ya sekondari ili waweze kunufaika na mpango wa serikali ya awamu ya tano wa elimu bila malipo.
Afisa Elimu Taaluma wa Halmshauri ya Mji wa Tarime Matiko John akifafanua jambo katika kikao hicho |
Mtendaji wa kata ya Turwa Mzurukwao akichangia hoja katika kikao hicho |
No comments:
Post a Comment