NEWS

Tuesday, 5 November 2019

NMB YATOA MSAADA KWA SHULE 3 RORYA




Benki ya NMB leo Oktoba 5,2019 imetoa msaada wa madawati 125, mabati 50 na  vifaa vingine vya ujenzi  wenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa shule tatu  zilizopo Wilaya ya Rorya Mkaoni Mara .Mkuu wa Wilaya ya Rorya(DC) Simon Chacha amepokea msaada huo ambao umekabidhiwa na  Amos Mubusi kwa niaba ya Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa katika hafla ambayo imefanyika katika shule ya msingi Minigo.


 “Napenda kuishukuru benki ya NMB kwa msaada huu wa madawati  na vifaa vya ujenzi kwa shule zetu hizi tatu”, amesema  Chacha.
Kwa upande wake Mubusi amesema msaada huo ni sehemu ya ushiriki unaofanywa na benki hiyo katika  kusaidia maendeleo ya jamii maeneo mbalimbali nchini.


Mubusi aliambatana na Meneja wa NMB tawi la Rorya Jackline Kapolesya.
Mbali na Minigo shule zingine zilizonufaika na msaada huo ni shule ya msingi Ryaghati na shule ya sekondari Katuri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages