NEWS

Saturday 9 November 2019

POLISI TARIMERORYA WAKAMATA AK47 BAADA YA KUKABILIANA VIKALI NA WATUHUMIWA WA UJAMBAZI
Na mwandishi wetu, Tarime
Jeshi la polisi katika Mkoa wa Kipolisi TarimeRorya limefanikiwa kupata siraha mbili ambazo moja ni AK47 na  ambayo imetengenezwa kienyeji lakini inatumia risasi za SMG baada ya kukabiliana vikali na watuhumiwa wa ujambazi katika eneo la Obwere, Shirati Wilayani Rorya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi TarimeRorya Henry Mwaibambe amewambia waandishi wa habari ofisini kwake leo Novemba  9, 2019 ofisini  kuwa  watuhumiwa watatu katika ya watano waliohusika katika tukio hilo wamefariki dunia.

Pia askari polisi waliokota risasi na maganda ya risasi kadhaa katika eneo la tukio , amesema kamanda  Mwaibambe.
“ Haikuwa kasi nyepesi  ilikuwa vita kali na risasi 60 zilizipigwa katika eneo la tukio”, amesema RPC Mwaimbambe .
Hivi sasa kamanda Mwaibambe amesema wanawasaka watuhumiwa wawili waliokimbia na siraha aina ya shortgun.
RPC Mwaibambe amesema siraha ya kienyeji waliopata ina mlio mkali kama wa mabomu .


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages