Na Mwandishi wetu,
Chui ambaye alikuwa amejificha
katika mashamba ameshambulia na kujeruhi watu sita katika kijiji cha Bisarara ,
Kata ya Sedeco Wilayani Serengeti Mkoani Mara leo asubuhi.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti
Nurdin Babu amesema hakuna mtu aliyepoteza maisha katika shambulio hilo la
chui.
“ Huyu chui alianza kusumbua
tangu saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nane mchana alipouawa." Babu ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu leo jioni.
Pongezi sauti mara habari
ReplyDelete