Toleo la kwanza la gazeti hilo ambalo litakuwa likitoka kila siku ya Jumatatu limetoka leo na limesambazwa katika mikoa ya kanda ya Ziwa ukiwemo Mkoa wa Mwanza. Gazeti hilo limeanzishwa na kampuni ya Mara Online.
Eng Msafiri amesema RC Malima amefurahishwa sana na uanzishwaji wa gazeti hilo hususani ni kauli mbiu yake ambayo ni Habari kwa Maendeleo .
“ Ni imani yetu kuwa gazeti hili litakuwa chachu ya maendeleo ya mkoa wa Mara “, amesema Eng Msafiri ambaye alifuatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Tarime.
Viongozi mbalimbali kutoka chama cha CCM na CHADEMA wakiwemo wawakilishi wa wabunge wa jimbo la Tarime Mjini na jimbo la Tarime vijijini, wadau wa maendeleo na viongozi wadini wamehudhuria uzinduzi huo ambao umefanyika katika Hoteli ya Goldland.
Mtendaji Mkuu wa Mara Online Jacob Mugini amesema gazeti mbali litakuwa likitoa habari ambazo zinahamasisha maendeleo na uhifadhi endelevu litakuwa na ukurasa maalumu kwa ajili ya kuonesha uzuri wa Mkoa wa Mara .
No comments:
Post a Comment