Mwanamume mmoja nchini Rwanda ambaye alikiuka amri ya kukaa nyumbani kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona, amefariki dunia baada ya kuuawa na mamba alipokwenda kuvua samaki.
Rwanda ambayo ina wagonjwa 41 iliwaambia wananchi wakae nyumbani kuepuka maambukizi. Meya wa Wilaya ya Kamonyi Kusini mwa Rwanda Alice Kayitesi, aliviambia vyombo vya habari kuwa mwanaume alikiuka sheria ya kukaa nyumbani, nakuwa miongoni mwa watu wachache ambao hawaonyeshi ushirikiano katika sheria hii ya kukaa nyumbani ili kuzuia kusambaa kwa corona.”
No comments:
Post a Comment