RAIS wa Tanzania Dkt John Magufuli
amesema kuwepo kwa ugonjwa wa Corona isiwe sababu ya watu kutishana kiasi cha
kumsahau Mungu.
Badala yake, Rais Magufuli amewataka
Watanzania kuendelea kuchapa kazi na kujenga uchumi huku wakizingatia maelekezo
ya kitaalamu ya kujikinga nao na kumwomba Mungu auepushe.
Aidha, amekemea tabia ya watu
wanaofanya mzaha juu ya ugonjwa huo na kuwatia hofu wananchi kupitia mitandao
ya kijamii.
Akizungumza katika ibada ya Jumapili
leo kwenye Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma
iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo, Padre Onesmo Wisi, Rais Mgufuli
amesema:“Watu tusitishane, tunatishana mno. Niwaombe ndugu Wakristo na
Watanzania kwa ujumla na madhehebu yote, huu ndio wakati mzuri sana wa kumtegemea
Mungu kuliko wakati wote, tuendelee kuchapa kazi, tuendelee kujenga uchumi
wetu, hatuwezi kusalimu amri kwa ugonjwa huu wa Corona na kushindwa kumtegemea
Mungu.”
No comments:
Post a Comment