Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani
Simiyu, Festo Kiswaga amewataka wananchi wilayani humo kuacha tabia ya kunawa
mikono kwenye chombo kimoja kama vile bakuli na beseni, badala yake watumie
maji yanayotiririka kuepuka maambukizi ya corona (COVID-19).
“Tusitumie bakuli moja kunawa mikono kwa
kuitumbikiza ndani, badala yake tumie maji yanayotiririka. Ndani ya
familia, hususan wakati wa kula ni vema kila mmoja anawe maji yake hata
kwa kumwagiliziana,” amesisitiza Kiswaga.
Aidha, Kiswaga amepiga marufuku michezo yote
na sherehe zinazofanyika katika mikusanyiko na kuwahimiza wananchi wote kufuata
maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya na serikali katika kuchukua
tahadhari dhidi ya janga hilo la kimataifa.
“Jikinge na corona, zingatia ushauri wa
wataalamu wa afya, afya yako, mtaji wako. Bariadi bila maambukizi ya corona
inawezekana,” amasema Kiswaga.
(Habari na Anita Balingilaki, Bariadi)
No comments:
Post a Comment