WAFANYABIASHARA
wengi jijini Mwanza wameendelea kuuza sukari kwa bei ya juu licha ya serikali
kutangaza bei elekezi ambayo ni kati ya Sh 2,600 na 3,000 nchini.
Uchunguzi
uliofanywa na Mara Online News leo Jumapili Aprili 26, 2020 katika baadhi ya
mitaa ikiwamo Uhuru, Liberty na Mitimirefu jijini hapa, umebaini uwepo wa
maduka yanayouza sukari kati ya Sh 3,200 na 3,500.
Hivi
karibuni Serikali ya kupitia kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent
Bashungwa, ilitangaza bei elekezi ili kudhibiti upandaji holela wa bei ya
sukari nchini.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Sukari Namba 20 ya Mwaka 2001 (kifungu cha 251) chini ya
kifungu cha 11A, waziri mwenye dhamana ya viwanda na biashara ana mamlaka ya
kutangaza bei ya kikomo ya bidhaa hiyo.
(Habari na
Suleiman Shagata, Mwanza)
No comments:
Post a Comment