Japokua dunia hivi leo inapambana
na janga la korona maisha hayana budi kuendelea.
Hili limedhibitishwa na hospitali
ya Praram 9 nchini Thailand ambapo tarehe 9 mwezi huu watoto wawili wachanga waliozaliwa
walivalishwa barakoa (masks) za kutengeneza pale pale hospitali katika hatua ya
kuwakinga na maambukizi ya virusi vya Corona wakiwa wanapelekwa nyumbani kutoka
hospitalini walipozaliwa.
Mama wa watoto hao awali alikua
ameiambia hospitali kua atatumia taxi au usafiri wa umma kwenda nao nyumbani
hivyo kupelekea manesi kuingia na hofu
juu ya usalama wa watoto wale ndiposa wakabuni na kutengeneza masks kwa ajili
ya kuwalinda kwa kipind hicho kifupi watokapo hospitali kuelekea nyumbani.
‘’Kinga za uso zilikua za muda
mfupi’’ hospitali ilisema…kinga izo zilikua za wale watoto tu sababu ya hofu ya
wao kua na hati hati ya kuambukizwa virusi hivyo kwenye usafiri na sio
kwa ajili ya watoto wote wanaozaliwa hapa’’ walimalizia.
Pia waliongeza kua wanajali zaidi
usalama.
Picha zilizopigwa kupitia kioo cha
hospitali zinaonesha manesi na mama wa watoto wale wakiwa wamevaa masks wakati
wamewazunguka.
Kituo cha Marekani cha kudhibhiti
na kuzuia magonjwa (CDC) kinapendekeza watoto wenye miaka miwili na zaidi kuvaa
masks wanapotoka kwenda kwenye hadhara ya watu ili kudhibiti kuenea kwa virusi
vya corona.Wataalam hao wanaamini kuwa watoto huambukizwa haraka na kusambaza
bila ya wao kufahamu.
Kwa mujibu wa CDC, mtoto mchanga ni rahisi
kuhusishwa na ueneaji wa virusi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine
‘’Idadi ndogo sana ya watoto wamepatikana na virusi
hivyo mda mfupi tu baada ya kuzaliwa…CDC walisema kwa tafiti na taarifa za
ujauzito na kunyonyesha…ingawaje haijajulikana kama watoto hao walipata kirusi
hicho kabla au baada ya kuzaliwa’’.
No comments:
Post a Comment