NEWS

Sunday 3 May 2020

KENYA YAREKODI IDADI KUBWA YA MAAMBUKIZI MAPYA YA CORONA KWA SIKU MOJA

Kenya imerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya corona kwa siku moja , kuwahi kushuhudiwa tangu kisa cha kwanza cha maambukizi hayo kilipotangazwa tarehe 12 Machi
Akitangaza upatikana kwa visa vipya 24 vya maambukizi ya corona Katibu mkuu katika Wizara ya Afya nchini Kenya Mercy Mwangangi jana Mei 2, amesema watu hao wamepatikana na Covid-19 kufuatia upimaji wa sampuli 1,195 katika kipindi cha saa 24.
Dokta Mwangangi amesema kuwa saba kati ya visa hivi vipya vilipatikana katika kitongoji cha jiji la Nairobi cha Kawangware kinachokaliwa na idadi kubwa ya watu. Idadi ya visa vipya vya maambukizi iliyopatikana kwa ujumla jijini Nairobi imefikia 20.
Katibu mkuu katika Wizara ya Afya nchini Kenya Mercy Mwangangi
Amesema 10 kati ya visa vipya vimepatikana katika eneo la Eastleigh jijini Nairobi huku watano wakitoka Mombasa na wawili kutoka Kuria West katika kaunti ya Migori.
Katibu huyo Mkuu wa Wizara ya Afria ametangaza pia kwamba mtu mmoja zaidi amekufa kutokana na virusi hivyo , na hivyo kuifanya jumla ya idadi ya vifo vya corona Kenya kufikia watu 22.
Wizara hiyo pia imeripoti kuwa watu wawili zaidi wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kukutwa bila virusi, na hivyo kuongeza idadi ya watu waliopona kufikia 152.
BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages