NEWS

Friday 1 May 2020

WANAHABARI WANEEMEKA NA VIFAA KINGA KUTOKA KWA DIWANI SIMIYUDiwani wa kata ya Nyashimo iliyopo wilayani Busega Mkoani Simiyu
 Mickness Mahela ametoa msaada wa vifaa kinga dhidi ya  maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) kwa waandishi wa habari wa mkoani humo lengo likiwa kuwakinga  wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.


Vifaa hivyo ni pamoja na ndoo mbili za kunawia mikono ,vitakasa mikono chupa 18 ,barakoa 46, sabuni za maji za kunawia mikono chupa 5 ,deltol chupa kubwa moja na tissue paper paketi 5 vikiwa na  thamani ya zaidi ya sh. 200,000 (laki mbili).

Akikabidhi vifaa hivyo Mahela amesema wanahabari ni moja ya kundi ambalo lipo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa corona pindi wanapokuwa kwenye majukumu yao, hali ambayo imemfanya kutoa msaada huo.
Diwani wa kata ya Nyashimo Mickness Mahela (Kulia)  akikabidhi vifaa kinga kwa waandishi wa habari Mkoani simiyu 


 Kama tujuavyo wanahabari ni moja ya kundi kubwa, ambalo linakutana na watu mbalimbali kutoka maeneo tofauti tofauti na wako hatarini kupata huu ugonjwa na mbali na kutoa elimu kwa jamii juu ya kujikinga na corona, lakini wao wanatakiwa kuwa na vifaa kujikinga,” amesema mahela.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya waandishi wa habari Mkoani humo, Makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu Paschal Michael amemshukuru diwani huyo kwa kutoa msaada huo na kuongeza kuwa wanahabari wako kwenye kundi hatari kutokana na kukutana na watu wengi zaidi.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Simiyu Derick Milton amemshukuru  diwani huyo huku akiwaomba wadau wengine kuendelea kujitokeza kusaidia vifaa kinga.(Habari na Anita Balingilaki, Bariadi)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages