MBUNGE
wa Viti Maalumu kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Amina Makilagi,
amekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo, mabati 100, shuka zaidi 100 na
saruji kwa ajili ya kituo cha afya Magena wilayani Tarime, vyenye thamani ya Sh
milioni saba.
Viongozi wa wilaya ya Tarime wakipokea msaada |
Makilagi
amekabidhi msaada huo jana Mei 15, 2020 kupitia kwa Kamati ya Siasa ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.
Mbunge
huyo pia alikabidhi msaada wa kompyuta moja kwa
ajili ya shule ya sekondari Bomani iliyopo Halmashauri ya Mji waTarime
(Habari an
Frankius Cleophace, Tarime)
No comments:
Post a Comment