MKUU wa Wilaya ya Tarime
mkoani Mara, Mhandisi Mtemi Msafiri, jana Juni 18, 2020 amesemea hatasaini
kupitisha malipo kwa ajili ya wananchi wa kijiji cha Komarera waliotegesha
mazao na miti kwa lengo la kulipwa fidia
kutoka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliopo Nyamongo.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime,
Mhandisi Mtemi Msafiri (mwenye fimbo) akikagua mazao yaliyotegeshwa katika
kijiji cha Komarera
Mhandisi Msafiri ametoa
msimamo huo alipotembelea eneo ambalo limefanyiwa tathimini na kushuhudia mazao
yaliyotegeshwa katika eneo hilo ndani ya muda mfupi baada ya wananchi kubaini
kuwa eneo hilo linahitajika kwa upanuzu wa shughuli za mgodi huo.
Aidha, mkuu huyo wa wilaya
ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwahoji wathamini
waliohusika kutathimini vitu vilivyotegeshwa katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime,
Mhandisi Mtemi Msafiri akionesha zao lililotegeshwa katika kijiji cha Komarera
Pia ameagiza Jeshi la
Polisi wilayani Tarime kumtia nguvuni Mwenyekit wa Serikali ya Kijiji cha
Komarera, Nyamganya Marwa, kwa anayetuhumiwa kuhamasisha wananchi kutegesha
mazao na miti katika eneo hilo.
Uthamini katika eneo hilo
umefanywa hivi karibuni na Kampuni ya Whiteknights Real Estates Investment Co. Ltd.
No comments:
Post a Comment