NEWS

Friday 19 June 2020

Misiwa: Wanatarime yajayo yanafurahisha



Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Moses Misiwa, amesema uamuzi wake wa kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) umezingatia maslahi mapana ya kimaendeleo kwa wananchi wa Tarime Vijijini.

"Wananchi wangu wawe watulivu kwani nimejiunga na chama tawala - CCM ili kuhakikisha tunapeleka maendeleo yetu kwa kasi kubwa kuliko tuliyokuwa nayo," amesisitiza Misiwa katika mahojiano na Mara Online News kwa njia ya simu leo Ijumaa Juni 19, 2020.

Misiwa ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Diwani wa Kata ya Nyamwaga kwa tiketi ya Chadema kwa miaka mitano sasa, ametangaza kujiunga na CCM jana Alhamisi, ambapo amepokewa na Katibu wa Kitaifa wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa chama hicho tawala, Humphrey Polepole.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages