Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA kimejaza nafasi iliyokuwa wazi ya mwenyekiti wa wilaya ya Tarime
kwa kumchagua Mwenyekiti wa Halmashauri yaTarime Hamis Nyanswi kuwa
mwenyekiti mpya wa CHADEMA katika wilaya hiyo
yenye majimbo mawili ya Tarime Mjini na Tarime vijijini.
Nyanswi(pichani anayeongea kushoto) amepata uhsindi wa kishindo kushika nafasi
hiyo katika uchaguzi uliofanyika leo 12 Juni 2020 katika ofisi ya wilaya ya chama hicho mjini Tarime.
Akitangaza matokeo msimamizi wa
uchaguzi huo Mahonia Joseph amemtangaza Nyanswi kuwa mshindi baada ya
kupata kura 18 kati 19 zilizopigwa .
Mshindani wake Jacob Kayelle
ameambulia kura moja.
No comments:
Post a Comment