NEWS

Tuesday 21 July 2020

Jafari Chege mshindi kura za maoni CCM Rorya


KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jafari W. Chege(pichani), ameibuka mshindi katika uchaguzi wa kura za maoni kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge jimbo la Rorya mkoani Mara.
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Jumanne Julai 21, 2020 kwenye viwanja vya ofisi ya CCM Wilaya ya Rorya, Chege ameshinda kwa kuvuna kura 152, idadi ambayo haikufikiwa na mgombea mwingine kati ya 49 waliochuana naye.#Mara Online News

3 comments:

  1. Hongera Sana comrade tunategemea mengi na makubwa kutoka kwako

    ReplyDelete
  2. Songa mbele kwa matumaini makubwa tuna matarajio ya ufanisi kutokana na njozi za vijana. Jimbo hilo lina mahitaji muhimu sana ya jamii kama maji safi, elimu bora kuanzia ngazi za chini na kuwafikisha watoto wetu elimu ya juu, hifadhi ya mazingira, kilimo bora na cha kisasa, ufugaji ulioimarishwa na kuboreshwa, utafiti wa madini, biashara yenye ufanisi, uinuaji na uwezeshaji wanawake na vijana kujitegemea na kuondoa utegemezi. KUPAMBA NA MILA POTOFU ZILIZOPITWA NA WAKATI. Na jitihada za makusudi za kupunguza umaskini. Wazee tutakuunga mkono

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages