NEWS

Saturday 29 August 2020

Kembaki, Matiko wachangia nyumba ya mchungaji SDA

Mchungaji Wlliam Gordson Mbunguni (kushoto) akiteta jambo na wagombea ubunge jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki (katikati) na Esther Matiko (kulia), mara baada ya kuwaombea kampeni njema.

 

WAGOMBEA ubunge katika jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki (CCM) na Esther Matiko (Chadema), leo Agosti 29, 2020 amechangia fedha na vifaa kufanikisha ujenzi wa nyumba ya mchungaji wa Kanisasa la Waadventista Wasabato (SDA) Mtaa wa Majengo mjini Tarime.

 

Katika harambee hiyo, Kembaki amechanga shilingi milioni mbili na Matiko ametoa mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni moja.

 

Mchungaji William Gordson Mbunguni amewaombea wagombea hao na kuwahimiza kudumisha upendo na kumtaguliza Mungu katika kampeni zao za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, 2020.

Mgombea ubunge katika jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki kwa tiketi ya CCM (kulia) akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya mchungaji wa Kanisa la SDA Mtaa wa Majengo ambapo alitoa shilingi milioni mbili kuchangia ujenzi huo.

 

“Tayari kati yenu Mungu anajua mbunge anayekuja,” Mchungaji Mbunguni amewaambia wagombea hao.

 

Baada ya kutoka kwenye harambee hiyo, Kembaki ameelekea katika Kanisa la SDA Sabasaba mjini Tarime ambapo pia ametoa shilingi milioni moja kuchangia maendeleo ya kanisa hilo. 

 

(Habari na picha zote na Mara Online News)

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages