NEWS

Monday 7 September 2020

Esther Matiko ajivunia matokeo chanya uzinduzi wa kampeni zake Tarime Mjini

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema) akizungumza na Mara Online News nyumbani kwake, juzi.

MGOMBEA ubunge Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema), ameelezea kupata faraja ya moyo kutokana na kile alichoita matokeo chanya ya mwitikio wa wakazi wa jimbo hilo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake.

 

Siku ya uzinduzi huo, yaani juzi Septemba 6, 2020 umati mkubwa wa wananchi ulimfuata Matiko nyumbani kwake eneo la Bomani na kumsindikiza hadi uwanja wa Serengeti mjini Tarime ulipofanyika mkutano wa uzinduzi, kisha kumsindikiza tena kurudi nyumbani kwake.

 

“Ni kumbukumbu ya kipekee, nimeona mrejesho wa kazi kubwa niliyowafanyia wana-Trime Mjini, siku zote wamekuwa na mwitikio chanya kwangu, uzinduzi wa kampeni zangu mwaka huu umekuwa na matokeo chanya zaidi, ni mara dufu ya ule wa mwaka 2015.

 

“Wananchi wamejitokeza kwa wingi wakajaza uwanja wa Serengeti, kulikuwa na shamrashamra kubwa na polisi wamekuwepo kwa ajili ya kulinda usalama, kwa kweli nimepata faraja sana,” amesisitiza mgombea huyo katika mahojiano maalumu na Mara Online News.

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini kwa tiketi ya Chadema, Esther Matiko akijinadi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni zake kwenye uwanja wa Serengeti mjini Tarime, juzi.


Katika kinyang’anyiro cha ubunge Tarime Mjini, Matiko ambaye anatetea nafasi hiyo anachuana kwa mara nyingine na Michael Kembaki (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, 2020.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages