NEWS

Tuesday 8 September 2020

Waitara awasha moto Tarime Vijijini

Waitara akiwa katika mapokezi kuelekea kwenye viwanja vya uzinduzi wa kampeni

 

MGOMBEA ubunge Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara leo Septemba 8, 2020 amezindua kampeni zake ambazo huenda zikaweka historia baada ya mamia ya wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Nyamwaga.

Waitara (katikati) akiwa na mke wake, Lucy (kulia) wakiwapungia wananchi mikono


 

Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI anaonekana kuwa na mvuto wa kipekee huku akiungwa mkono na watu wa kada mabalimbali wakiwemo wazee, vijana na wanawake.

Waitara akipokewa na wananchi na wanachama wa CCMViongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye (Namba Tatu) wamehudhurulia uzinduzi huo.

Kikundi cha ngoma ya Kikurya kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya WaitaraDuru za kisasia zinasema Waitara ambaye kipindi kilichopita alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam anatarajiwa kutoa ushindani mkali kwa washindani wake ambao ni Charles Mwera wa ACT – Wazalendo na John Heche (Chadema) anayetetea nafasi hiyo.

Kada wa CCM, Mariama Mkono akionesha furaha yake Waitara akizindua kampeni zake leoHeche alizundua kampeni zake katika mji mdogo wa Sirari, wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages