NEWS

Thursday 10 September 2020

Mgombea ubunge Bariadi, Mhandisi Kundo Andrea ajionea kero za wananchi

Mhandisi Kundo Andrea akijionea kero za wananchi wa jimbo la Bariadi

HUKU akielekea kwenye uzinduzi wa kampeni zake za ubunge katika jimbo la Bariadi mkoani Simiyu, Mhandisi Kundo Andrea tayari ameshazungukia kata 24 kati ya 31 zinazounda jimbo hilo kujionea kero za wananchi.

 

Akiwa katika kata za Mhango, Sakwe na Itubukilo leo Septemba 10, 2020, Mhandisi Andrea anayegombea ubunge kwa tiketi ya CCM, amesema amejionea kero kadhaa ikiwemo adha inayowakabili wananchi katika kuvuka mto Mgudama, hasa misimu ya mvua.

 

Mgombea huyo amesema ameamua kuzungukia kata hizo kabla ya uzinduzi rasmi wa kampeni zake ili aweze kuweka ahadi zenye tija kwa wananchi.

Hapa Mhandisi Kundo Andrea (wa kwanza kushoto juu) akiwa na baadhi ya wananchi katika ziara yake ya kujionea changamoto zinazowakabili wakazi wa jimbo la Bariadi

 

Mhandisi Andrea amebainisha kuwa anatarajia kuzindua rasmi kampeni zake Septemba 17, 2020 na kwamba mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

 

“Sipendi kuletewa taarifa za changamoto za wananchi bali napenda kujionea mwenyewe ili kujua namna ninavyoweza kutatua kero hizo,” amesema.

 

(Habari na picha zote na Anita Balingilaki, Bariadi)

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages