NEWS

Friday, 17 October 2025

Tarime Mji: Shule ya Msingi Azimio yawatunuku wadau wake vyeti vya shukrani



Mfanyabishara wa mjini Tarime, Mesti Heche, akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Shule ya Msingi Azimio jana Oktoba 16, 2025.

Na Mwandishi Wetu
Tarime
-------------

Shule ya Msingi Azimio ambayo iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime jana Oktoba 16, 2025 aliwatunuki vyetu vya shukrani wadau ambao wamekuwa wakiunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kuboresha mazingira ya kujifuzia katika shule hiyo.

Wadau waliotunukiwa vyeti hivyo ni mfanyabiashara wa mjini Tarime, Mseti Heche ambaye ameipitia shule hiyo msaada wa viti 20 na photocopy machine na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Tarime na Diwani wa Kata ya Nyakonga, Simion Kiles “K”, kwa kuendelea kuwa mmoja wa wadau wanaofanikisha wanafunzi na walimu wa shule hiyo kufanya ziara za mafunzo katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.


Mwakilishi wa “K”, Chale ‘Nyama’, akipokea cheti cha shukrani.

Kwa upande wake mwanahabari na Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mara Online, Jacob Mugini, alitunikiwa cheti kutambua mchango wa meza nne za walimu na ‘desk computer’ ambavyo aliipatia shule hiyo miaka michache iliyopita.


Mwanahabari ambaye pia ni CEO wa Mara Online, Jacob Mugini, akipokea cheti cha shukrani.

Huku kampuni ya Sota One Limited ilitunukiwa cheti kutambua mchango wake wa kuwezesha wanafunzi wa shule hiyo kupata chakula wanapokuwa shuleni.


Mwakilishi wa Soya One Limited, Mwita Meck, akipokea cheti cha shukrani.

Hafla hiyo ilifanyika katika shule hiyo ambapo pia ilihudhuriwa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini kupitia CCM, Esther Matiko, ambaye aliahidi kuipatia shule hiyo laptop na printer.


Esther Matiko (kushoto), akiteta jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Azimio, Rafael Bujiku.

Wadau hao waliahidi kuendelea kuunga mkono maendeleo ya elimu katika shule hiyo.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rafael Bujiku, aliwashukuru wadau hao kwa kuendelea kuwa wadau wazuri wa maendeleo ya shule hiyo.


Mseti Heche (wa pili kulia) akikabidhi viti 20 na kompyuta moja (haipo pichani) kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Azimio, Rafael Bujiku (katikati waliosimama mbnele). Waliosimama nyuma ni walimu wa shule hiyo.


Mwanahabari ambaye pia ni CEO wa Mara Online, Jacob Mugini, akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages