NEWS

Sunday 6 September 2020

Wagombea wa ACT, NCCR wajiondoa ubunge Serengeti, watimkia CCM


 

WAGOMBEA ubunge kwa tiketi ya NCCR - Mageuzi na ACT – Wazalendo katika jimbo la Serengeti mkoani Mara wamejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho na kujiunga na CCM leo Septemba 6, 2020.

 

Wagombea hao ni Amos Babere Roswe (ACT-Wazalendo) na Daniel Daudi (NCCR- Mageuzi).

 

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Serengeti, Mhandisi Juma Hamsini, amethibitisha kupokea barua za kijiondoa kwa wagombea hao wawili katika king’anyiro hicho.

 

Mchuaono wa ubunge katika jimbo hilo sasa umebaki kati ya Amsabi Jeremiah (CCM) na Catherine Ruge (Chadema).

 

Taarifa zaidi kutoka Serengeti zinasema mgombea kupitia CCM amezindua kampeni zake za ubunge leo Septemba 6, 2020.

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages