NEWS

Saturday 5 September 2020

Madaraka Nyerere awaomba Watanzania kumchagua Magufuli

Madaraka Nyerere akimwombea Dkt John Magufuli kura za urais leo Septemba 5, 2020 mjini Musoma, Mara

 

MTOTO wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Madaraka Nyerere, amewaomba Watanzania kwa ujumla kumchagua Dkt John Magufuli kuendelea na nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili aendelee kuipaisha zaidi Tanzania kiuchumi.

 

“Ninawaomba Watanzania wote tumchague Dkt John Pombe Magufuli aendelee kuwa Rais wetu kwa sababu amefanya kazi kubwa na nzuri sana katika kujenga uchumi wa nchi yetu na kwa umakini mkubwa sana,” amesema Madaraka.

 

Amesema kitendo cha Rais Magufuli kupaisha uchumi wa Tanzania kimemuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye alitamani kuona hatua hiyo ikifikiwa nchini.

Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere (kulia) akisalimiana na Rais Dkt John Magufuli katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, mjini Musoma, leo Septemba 5, 2020

 

Madaraka ameyasema hayo alipopewa nafasi ya kuzungumza katika mkutano mkubwa wa kampeni uliohutubiwa na Dkt Magufuli mjini Musoma, leo Septemba 5, 2020.

 

Madaraka amefuatana na kaka yake, Makongoro Nyerere na mama yao, mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere ambapo kila mmoja alipewa nafasi ya kumwombea Dkt Magufuli kura za urais kupitia uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

 

(Imeandikwa na Mara Online News, Musoma)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages