NEWS

Friday 20 November 2020

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, wanahabari wabeba rasilimali za maji

Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na maofisa wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria katika picha ya pamoja leo asubuhi mara baada ya ufunguzi wa warsha iliyoandaliwa na Bodi hiyo ikilenga kuimarisha ushirikiano baina yao katika kuhamasisha matumizi na uhifadhi endelevu wa rasilimali za maji ndani ya Bonde hilo.

 

BODI ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB) imeeleza azima yake ya kushirikiana na vyombo vya habari kuhamasisha matumizi na uhifadhi endelevu wa rasilimali za maji.

 

Katika kutekeleza azima hiyo, LVBWB imekutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na waandishi wa habari katika warsha iliyofanyika jijini Mwanza, leo Novemba 20, 2020.

 

“Wahariri wa yyombo vya habari ni wadau muhimu katika utunzaji wa vyanzo vya maji,” amesema Kaimu Mkurugenzi wa LVBWB, Renatus Shinhu, katika warsha hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Renatus Shinhu, akifungua warisha hiyo.

 

Mada mbalimbali zimewasilishwa na wataalamu ambayo ni wakuu wa vitengo katika ofisi ya LVBWB ambapo pia kulikuwa na mada kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika utunzaji wa vyanzo vya maji.

Mjiolojia Mwandamizi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Mhandisi Emmanuel Kisendi, akiwasilisha mada katika warsha hiyo.

 

Mkuu wa kitendo cha tathmini na ufuatiliaji wa rasilimali za maji katika Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Mangasa Ogoma, akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo.


Mkuu wa kitengo cha tathmini na ufuatiliaji wa rasilimali za maji katika Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Mangasa Ogoma, amesema watatumia waandishi wa habari kutatua changamoto zilizopo ikiwemo ya uchafuzi wa vyanzo vya maji.

 

“Ninyi [wahariri/waandishi wa habari] ni kama daraja, bila ninyi hatuwezi kufika,” amesema Ogoma.

Afisa Uhusiano wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Mhandisi Gerald Itimbula, akiwasilisha mada katika warsha hiyo.

 

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa LVBWB, Mhandisi Gerald Itimbula, amesema usimamizi endelevu wa vyanzo vya maji ni muhimu kwa ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla.

 

LVBWB ni taasisi inayoshughulika na usimamizi wa rasilimali za maji, kutunza, kulinda na kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji katika Bonde la Ziwa Victoria.

 

{Habari na picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages