NEWS

Monday 16 November 2020

Makamishna wa Uhifadhi TANAPA wang’arisha Serengeti Safari Marathon

Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Dkt Allan Kijazi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili (wa pili kushoto), Kamishna Msaidizi wa TANAPA Kanda ya Magharibi, Martin Loiboki (kulia) na washiriki wengine wa mbio za Serengeti Safari Marathon 2020, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA).

 

MBIO za Serengeti Safari Marathon zilizofanyika Novemba 14, 2020 ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) ziling’arishwa na viongozi mbalimbali wakiwamo kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) - ambao walishiriki kukimbia kilomita kadhaa.

 

Viongozi hao ni pamoja na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Dkt Allan Kijazi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa TANAPA Kanda ya Magharibi, Martin Loiboki na Mhifadhi Mkuu wa SENAPA, Masana Mwishawa.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kulia), Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Dkt Allan Kijazi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii (wa pili kulia), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Daniel Shilla (wa pili kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa TANAPA Kanda ya Magharibi, Martin Loiboki (kushoto), wakijadili jambo kabla ya kuanza mbio za Serengeti Safari Marathon ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), juzi.

 

Aidha, viongozi wa Serikali wakiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Calorine Mthapula na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Daniel Shilla - waliungana na viongozi hao wa uhifadhi wa wanyamapori katika mbio hizo.

Washiriki mbalimbali wakiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (mwenye jaketi nyekundu), Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Dkt Allan Kijazi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii (wa pili kutoka mwenye kofia ya bluu kulia) na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa TANAPA Kanda ya Magharibi, Martin Loiboki (wa tatu kutoka kwa Malima - waliosimama), wakijiandaa kuanza mbio za Serengeti Safari Marathon ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), juzi.

 

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (wa mbele kushoto) na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Dkt Allan Kijazi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii (wa mbele kushoto kwa Malima), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Danie Shilla (nyuma ya Malima) na washiriki wengine wa mbio za Serengeti Safari Marathon ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), juzi.

 

Kwa upande mwingine, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess, Msimamizi wa miradi ya wafadhili wa Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) Tanzania, Michael Thompson na Meneja Mradi wa FZS Tanzania, Masegeri Rurai, walishiriki mbio hizo za Serengeti Safari Marathon ambazo mgeni wake rasmi alikuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Tanzania, Jakaya Kikwete.

 

Mgeni rasmi wa mbio za Serengeti Safari Marathon 2020, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano, Jakaya Kikwete (wa pili kushoto), akiongozwa na wakuu wa mikoa, Adam Malima wa Mara (wa pili kulia) na Anthony Mtaka wa Simiyu (kushoto), ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) zilikofanyika mbio hizo.


Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess (wa nne kulia), Msimamizi wa miradi ya wafadhili wa Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) Tanzania, Michael Thompson (wa tatu kulia), Meneja Mradi wa FZS Tanzania, Masegeri Rurai (wa tano kulia) na wafanyakazi wengine wa shirika hilo ni miongoni mwa washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon zilizofanyika ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), juzi.

 

Washiriki wengine wa mbio hizo walikuwa watalii wa kigeni kutoka mataifa tofauti na watalii wa ndani kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mara, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam.

 

Lengo la mbio hizo za Serengeti Safari Marathon ni kuhamasisha utalii na uhifadhi wa wanyamapori na ikolojia ya Serengeti.

 

(Habari na picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages