NEWS

Tuesday 24 November 2020

Mbunge Kembaki aanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo Tarime Mjini

Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki, akizungumza wakati wa ziara yake ya kuchangia maendeleo ya shule za msingi jimboni humo leo.

 

MBUNGE wa Jimbo la Tarime Mjini, Michael Kembaki, leo Novemba 24, 2020 ameanza rasmi kutekeleza sehemu ya ahadi zake kwa vitendo ali[pofanya ziara katika shule za msingi za Nyamisangura, Tarime, Gamasara na Mwibari. 

 

Katika ziara hiyo, Kembaki ametoa Sh milioni 8.2 kwa ajili ya kugharimia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Nyamisangura na Tarime. 

Mbunge wa Tarime Mjini, Michael Kembaki akipitia mahitaji ya shule za msingi alizotembelea leo kabla ya kuchangia gharama za mahitaji hayo.

 

Kembaki ambaye alionekana kuguswa na tatizo la ukosefu wa vyoo katika shule hizo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliompatia ushindi, ametaka wahusika kujenga vyoo hivyo haraka iwezekanavyo. 

 

Amesema ameelekeza fedha ambazo angetumia kufanya sherehe ya kujipongeza baada ya ushindi kutatua kero ya ukosefu vyoo katika shule hizo. 


Mbunge huyo pia amechangia Sh milioni 5.4  kugharimia ujenzi wa vyoo vya walimu katika Shule ya Msingi Gamasara ambapo pia amekagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuahidi kusadia uboreshaji. 

Mbunge wa Tarime Mjini, Michael Kembaki akizungumza na wanafunzi na walimu wakati wa ziara yake ya kuchangia maendeleo ya shule za msingi jimboni humo leo.

 

Kembaki pia amechangia Sh milioni tano kuunga mkono juhudi za wananchi katika ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi Mwibari. 

 

Katika ziara hiyo, Mbunge Kembaki amefuatana na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Hamis Mkaruka ambaye ameshauri fedha za maendeleo ya mfuko wa jimbo kutumika vizuri kwa kugharimia uboreshaji wa huduma za jamii. 

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages